GET /api/v0.1/hansard/entries/736650/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 736650,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/736650/?format=api",
"text_counter": 283,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Machira",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 769,
"legal_name": "Jane Agnes Wanjira Machira",
"slug": "jane-agnes-wanjira-machira"
},
"content": "Huu si wakati wakulaumiana lakini ni wakati wa kuangalia kama Wakenya wako na chakula cha kutosha. Tukiangalia wakati uliopita, ufisadi umechukua sehemu kubwa zaidi. Wengine wameweka pesa kwa magunia na kuzificha katika godoro wanazolalia ndani ya nyumba. Hakuna pesa ambazo zinazunguka nchini. Hakuna hata uajiri. Kwa hivyo, lazima tuuangalie upande wa ufisadi. Lazima jukumu la sheria liwepo. Tumewaweka pale watu wa sheria ili wachukue lile jukumu sawasawa na kwa ukamilifu. Nikimalizia, ningependa kusema ya kwamba Kenya inaweza kujipatia chakula ikiwa kuna mikakati ambayo itatengenezwa na zile ofisi zote zinazohusika na ukulima na ushuru. Hizo zote zikihusika, tunajua chakula chaweza kupatikana Kenya. Hatuwezi kuwa tunapuuza mambo yale yaliyo muhimu. Juzi, tuliona watu walio na mishahara midogo wakiongezewa asilimia 18. Lakini hiyo mishahara midogo ndio tutakata tena ushuru. Watu hao kweli wataweza kununua unga? Hawawezi kununua unga. Kwa hivyo, lazima tuyaangalie zaidi mambo mengine katika kutafuta ushuru. Ni kina nani twawakata ushuru huu na twatoa kodi wapi? Lazima tuangalie kwa sababu yule mwananchi wakawaida ambaye anaongezewa hizo asilimia 18 ndio pia mwanzo anakosa hata pakiti ya unga. Hata pakiti ya unga hawezi kununua. Lazima tuangalie kama tumemaliza yote katika maghala yetu. Tukimaliza yote katika maghala yetu, tafadhali tuangalie huko nje kama tunaweza kupata mahindi kwa bei nafuu ambayo hatutakuwa tumefungua mlango mwingine wa ufisadi. Bali na hayo, naunga mkono Mswada huu."
}