GET /api/v0.1/hansard/entries/737263/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 737263,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/737263/?format=api",
"text_counter": 52,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Mheshimiwa Spika, asante kwa kunipa nafasi hii. Naomba niunge mkono Hoja hii tukiangalia kuwa tarehe 23 mwezi wa Mei itakuwa ni siku muhimu sana kwa Wabunge ama watu wote ambao wanatarajia kuomba viti tofauti tofauti, tukianzia na cha ugavana - ambacho nitakuwa nakiomba kwa watu wa Taita Taveta - maseneta, wabunge na wabunge wa kaunti. Mhe. Spika, ni muhimu tuwapatie Wabunge nafasi wahudhurie vikao hivyo kwa sababu ni mengi yatakuwa yanaelezwa. Wasipopata maelezo sahihi siku hiyo, huenda wengine wakashindwa kuwasilisha makaratasi yao ama vyovyote ambavyo vinahitajika na IEBC siku hiyo. Kwa hiyo, naomba tukubaliane zote, Wabunge, kwa kauli moja bila kupinga, tusiwe na kikao hapa Bungeni siku hiyo. Tupatiwe nasafi, twende mashinani, twende kwa kaunti zetu; tuelezwe wazi wazi ni nini kinahitajika. Ukiniambia niwe Bungeni siku hiyo na mimi natarajia kuwa gavana wa Taita Taveta - na wenzangu hawa wote wanatarajia wawe magavana ambao wanastahili - si vyema. Tumekubaliana kuwa hatutaaibisha Bunge hili. Wenzetu Wabunge ambao wanaomba viti vya The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}