GET /api/v0.1/hansard/entries/737380/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 737380,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/737380/?format=api",
"text_counter": 169,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Asante Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia Hoja iliyo mbele yetu. Kwanza kabisa, nimesimama kuunga mkono Ripoti hii kwa sababu mimi ni mwanachama wa Kamati ambayo imetayarisha na kuileta Ripoti hii mbele yenyu. Kufikia sasa, hakuna tetezi lolote kuhusu ugavi wa nafasi za Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki. Muungano wa vyama vya Jubilee imepewa nafasi tano na muungano wa vyama vya CORD umepewa nafasi nne. Kwa bahati mbaya, waaniaji wa kujisimamia ni wachache na hawakupata nafasi. Hapo hakuna tetezi. Tetezi letu liko wapi? Liko kwa mchakato wa vipi tutagawanya nafasi hizi kwa Wakenya kwa njia halali. Kwa nini nasema hivyo? Katika Ripoti hii, upande wa CORD, Wakenya 41 wameomba nafasi waweze kupewa fursa wawakilishe Kenya katika Bunge la Afrika Mashariki. Ukiniruhusu nitasoma barua ya pili. Barua hii imeandikwa na Seth Ouma Omolo kwa Kimombo. Ningependa kusoma barua hii kwa ruhusa yako. Inasema hivi: “I, hereby, seek that the Wiper Democratic Party submits at least two names to Parliament for election as is the spirit of Rule 6(1) on the number of nominees of each party, otherwise, subjecting the voters, Hon. Members of Parliament, to an election---”"
}