GET /api/v0.1/hansard/entries/737557/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 737557,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/737557/?format=api",
    "text_counter": 64,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Mhe. Spika, ukiangalia hali Wabunge walivyo, hawana nia ya kuendelea na Hoja kama hii. Najua hii Hoja ni ya mbinu ambazo zinatakiwa kutumiwa. Wabunge wamechoka, wamelemewa; wanataka haya mambo yaishe twende tufanye mambo mengine. Lakini, ukweli wa mambo ni kuwa hii Hoja ya mbinu imeletwa hapa kwa kutokubaliana kwa Kamati ile iliyokuwa imeundwa; inatuletea shida bure tu. Naomba tuangalie sheria zetu kwa sababu hili Bunge ndilo linatakiwa kutatua hili tatizo, vile Mwenyekiti amesema. Kwa hivyo, tusianze kuzungushana merry-go-round kila pahali. Naomba tukubaliane huu muda upunguzwe vile tulivyoomba. Tukishamalizana nao, ikileta shida hivyo hivyo, tuamue kwa hili hili Bunge. Labda, Wabunge lazima waweke sahihi kabisa kuwa hili Bunge ndilo linaheshimiwa na litoe muelekeo kwa wenzao. Naomba kuunga mkono."
}