GET /api/v0.1/hansard/entries/737656/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 737656,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/737656/?format=api",
"text_counter": 163,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kipyegon",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1453,
"legal_name": "Johana Ngeno Kipyegon",
"slug": "johana-ngeno-kipyegon"
},
"content": "Hao watu wametuzoea. Hii kashfa ya NYS tunataka iishe kwa sababu tumeiweka kwa Meza ya Bunge. Tunataka mashirika ya kiserikali kama vile Ethics and Anti-Corruption Commission (EACC), Director of Public Prosecutions (DPP) na Criminal Investigation Department (CID) waingilie haya maneno na wafanye upelelezi mara moja. Wale ambao walihusika wapelekwe kortini na kufunguliwa mashtaka. Kuna mtu ambaye anaitwa Wambora aliyefanya tenda ya Kshs79 milioni ya kutengeneza barabara ya kilometa tatu na nusu. Badala ya kulipwa hizo Kshs79 milioni za wizi, alilipwa Kshs791 milioni na Wakenya wanaona kwa kioo. Natamani Kenya ingekuwa kama Uchina kwa wiki moja na watu wawekwe kwa firing squad ndio wajue hiyo ni pesa ya raia na hatutaki waumie."
}