GET /api/v0.1/hansard/entries/737733/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 737733,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/737733/?format=api",
"text_counter": 240,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kombe",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 250,
"legal_name": "Harrison Garama Kombe",
"slug": "harrison-kombe"
},
"content": "Asante Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nichangie mjadala huu wa taarifa hii. Nimesoma na nimesikiza kwa makini wenzangu wakijadili. Lakini yapasa pia tuwe na shukrani kwa Mwenyezi Mungu na hata kwa Serikali iliyoko wakati wa sasa. Tukichukua mfano wa Kibra kama alivyosema Mhe. Ken Okoth, amekubalia hata ijapokuwa uchafu fulani ulikuwa ukiendelea katika Wizara, huduma hii ya taifa imebadilisha kiwango kikubwa eneo Bunge la Kibra. Na sio eneo la Kibra pekee yake ambalo limepata kubadilika, hata maeneo mengine hasa kwa upande wa tabia ya vijana maana wanapata mafunzo mbali na kazi ile wanafanya. Wanapata mafunzo ambayo ni ya kuwawezesha kuishi wakiwa ni wakenya wema. Hivi ninavyozungumza, huduma hii iko ndani ya Magarini. Na ningetaka kumfahamisha mwenye anasema ya kwamba nafanya kipindi changu cha tatu, kama ni juzi ni sawa lakini ukweli sharti usemwe. Rekodi zile ambazo zinatumika kwa utendajikazi wa huduma hii ya vijana ni hali ngumu sana kwamba utapata jina moja likaweza kurudiwa mara kumi kama mwengine alipotangulia kusema ili ipate kulipa watu tofauti tofauti. Hivi ninavyozungumza, kuna jambo ambalo limetutatiza katika Magarini kwa sababu hauwezi kutumia kitambulisho cha mtu mwingine kupata pesa na baadhi ya vijana walikuwa wametumia vitambulisho vya wazazi wao. Vitambulisho vile vya wazazi wao haviwezi kutambuliwa katika zile mashine za kuchukulia vidole; biometric . Kwa hivyo, ni lazima kitambulisho kiwe ni chako, laini ya M-pesa iwe ni yako na umeisajili kwa jina lako. Haiwezekani hata kwa Safaricom kwamba jina hilo moja litaweza kurudiwa rudiwa zaidi ya mara kumi. Hayo ni maneno ya uongo. Nawauliza Waheshimiwa Wabunge wenzangu kwamba panapo ukweli na panapo onekana kwamba kazi imefanyika, ni lazima tuwe na shukrani. Sio kwamba kila wakati tutakaposimama tunalaumu. Nashangazwa. Tumekuwa tukilia juu ya baa la njaa. Watu wanalalamika bei ya unga. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}