GET /api/v0.1/hansard/entries/737740/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 737740,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/737740/?format=api",
    "text_counter": 247,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Kombe",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 250,
        "legal_name": "Harrison Garama Kombe",
        "slug": "harrison-kombe"
    },
    "content": "Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kama anavyosema Mhe. Ken Okoth, ahadi zilikuwa kima cha ndovu lakini kilichotendeka ni kima cha sungura. Sawa, hicho kima cha sungura hakikuwepo mbeleni. Unastahili kuwa na shukrani. Ieleweke kwamba kuanza jambo si kazi rahisi. Huwa kuna changamoto nyingi unapoanzisha jambo. Kuna uwezekano kwamba yote yaliysajiliwa hapa yalitendeka. Lakini kufikia hivi sasa tunapozungumza, hali imerekebishika. Nimesema kutoka mwanzo kwamba naunga mkono Ripoti hii na ningependa hatua za kisheria zichukuliwe kwa waliohusika. Pamoja na hayo, ninasisitiza kwamba mabadiliko yale ambayo yameletwa na huduma hii ya vijana kwa taifa sharti tuyapongeze. Kazi yao inaonekana kote nchini. Ningependa kuzungumzia unga. Baa la njaa halikuanza jana ila mtu aliona mapema hali ambayo iliwapata Wakenya kisha akachukua hatua. Eti mahindi yaliyoagizwa juzi yalifika jana kwenye bandari yetu ya Mombasa! Kuna shida gani na hilo? Lililo muhimu ni lipi? Watu wetu wapate kupona ama waendelee kuangamia kwa njaa? Sharti Wakenya wajifunze kushukuru kwa mambo mazuri yanayotendwa. Sasa hivi, ifahamike kwamba NYS haikuanza wakati wa Jubilee. Imekuweko hata katika serikali za hapo awali. Kwa hivyo, yale yote ambayo yametendeka ni mabadiliko. Yameonekana wazi. Ni wajibu wetu kuboresha hii huduma. Ninaamini kwamba wale ambao wamechaguliwa hivi sasa kuongoza ugatuzi watawajibika na watafuatilia matumizi mazuri ya pesa za NYS. Hilo likitendeka sote tutashukuru. Kila mtu abebe msalaba wake. Atakayepatikana na hatia, basi sharia ichukue mkondo wake. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}