GET /api/v0.1/hansard/entries/738213/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 738213,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/738213/?format=api",
    "text_counter": 56,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "May 25, 2017 SENATE DEBATES 9 Sen. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika, naunga mkono ombi lililoletwa na Gavana wa Kisii, Mheshimiwa Ongwae, kwa sababu angependa kutumia ardhi hiyo kujenga majengo ambayo yatafaidi umma siku zijazo. Kuhusu ombi la Makueni, ningependa kusema kuwa nitaenda nyumbani shingo upande tutakapomaliza kipindi cha Bunge hili kwa sababu sijaona gavana hata mmoja akipelekwa jela na kufungwa. Wanaiba usiku na mchana na bado wanatembea barabarani. Wengi wao wamepata vitambulisho na tiketi za kuwania uchaguzi. Huo ni wizi mtupu. Bw. Spika, Bunge hili na mengine yatakayokuja yanafaa kuhakikisha kuwa kazi inafanyika na kuona kwamba mali ya umma inatunzwa."
}