GET /api/v0.1/hansard/entries/739893/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 739893,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/739893/?format=api",
    "text_counter": 377,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Ngunjiri",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1179,
        "legal_name": "Onesmas Kimani Ngunjiri",
        "slug": "onesmas-kimani-ngunjiri"
    },
    "content": "Jambo ambalo liko mbele yetu ni la kuweka mikakati, sheria za kusaidia na kuleta wadau wa pande zote pamoja ili tupitishe mikakati mizuri kuhusu maji ambayo itasaidia Kenya. Hata imechelewa. Hii Hoja ingeletwa kitambo ili itusaidie sisi wote. Tuko na bwawa moja ambalo limetengenezwa juzi na Serikali. Nimesikia kwamba wanataka kutengeneza mabwawa katika kila eneo bunge. Katika eneo bunge la Bahati, tulikuwa na shida ya maji sana. Tuko na mabwawa machache na watu wa Bahati wameanza kusherehekea kwa sababu wataanza kupata maji mazuri. Huko Bahati tuko na mabwawa ambayo yalitengenezwa wakati wa mbeberu karibu miaka sitini iliyopita. Lakini hayo mabwawa hayajaundwa upya ili yaweze kuteka maji mengi kwa sababu watu wameongezeka. Naunga hii Hoja mkono na najua Wakenya watafurahia tukiipitisha na kushirikiana ili tuweke mikakati na sheria nzuri kuhusu maji."
}