GET /api/v0.1/hansard/entries/740095/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 740095,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/740095/?format=api",
"text_counter": 102,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Kwa hivyo, nashukuru Mhe. Benjamin Langat amekuja akasema wazi kuwa bado yuko na anaendelea. Wakati umefika wa kuambiana ukweli na ukweli ujitoe wazi. Tukiwa tunaleta mabadiliko katika Hoja yoyote Bungeni, hasa ambayo inahusu fedha, ni lazima na ni muhimu vipengele vyote vya sheria vifuatwe. Kama tutakaa hapa na watu watumie mamlaka ambayo hawana na yakubalike kuwa sheria ipitishwe kiholela, tutakuwa tumehujumu nchi yetu na tutaepuka mamlaka tuliyopewa na wananchi. Nikimalizia, nasema hivi: Wakati huu tufuate sheria vile ilivyo. Kama Waziri ambaye anahusika na mambo na fedha hakuhusishwa kulingana na sheria, tunaomba ahusishwe kikamilifu na iletwe tena na ijadiliwe vile inavyotakikana. Wale ambao wamejitwika mzigo wa kubeba mamlaka ambayo si yao wakome. Tuelezane wazi wazi. Kwa haya machache, kama ujuavyo, hivi nakunja jamvi langu. Labda haya yatakuwa mazungumzo yangu ya mwisho mbele ya Wabunge wenzangu. Naomba Bunge liendelee kuheshimu Katiba na sheria zake. Ahsante."
}