GET /api/v0.1/hansard/entries/740603/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 740603,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/740603/?format=api",
    "text_counter": 197,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Mengi yamesemwa kuhusu mabadiliko kwenye Katiba ya Kenya kuhusu suala la viti vya Bunge la Taifa, Seneti, pamoja na mabunge ya kaunti. Ukweli ni kwamba, Wakenya bado wana tatizo la kuchagua akina mama, walemavu na vijana. Mila na desturi za Wakenya ni kuwa kuna viti vinafaa jinsia ya waume na vingine vya sisi wajinsia ya kike tunaagaliwa kijadi katika maeneo yetu. Lakini inawezekana akina mama wanachaguliwa kwa sababu nimechaguliwa mara ya tatu sasa. Inawezekana kuwa si mimi peke yangu. Kuna wengine pia ambao wamechaguliwa hapo mbeleni kama dada yangu Millie Mabona, Martha Karua, Charity Ngilu na Beth Mugo. Wengi wamechaguliwa lakini sio wengi vile inavyotakikana kwa mujibu wa Katiba yetu ya Kenya."
}