GET /api/v0.1/hansard/entries/740604/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 740604,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/740604/?format=api",
"text_counter": 198,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "Kipengele cha 90(7) na (8) kinazungumuzia umuhimu wa kuwa na akina mama na hata kikaweka makusudio ya kuwapatia viti ambavyo watagombea wenyewe kwa wenyewe ili tuweze kuongeza idadi yao kwa viti vya uchaguzi. Lakini vile vile, tukiangalia Kipengele cha 81 kinazungumizia umuhimu wa kuwa kwenye Bunge la Taifa na za bunge za kaunti, watu wa jinsia moja wasipite thuluthi mbili ya jinsia ili thuluthi ya tatu iweze kupatiwa wale wanyonge ambao hawawezi kupata nafasi wakati wa uchaguzi. Viti hivi ambavyo vilitengwa kwa ajili ya akina mama viliwekwa pale kwa makusudio ya kuwa watu watavitumia kwa muda wa miaka mitano na baada ya hapo wanaweza kugombea nafasi za maeneo bunge ambazo ni 290. Lakini, kama tulivyoona juzi katika mchujo, kuna akina mama wapya waliochaguliwa. Wengi waliokuwa kwenye viti vile hawakuweza kupatiwa nafasi kuendelea kupigania. Wengi ambao walijaribu viti vya maeneo bunge 290, hawakupatiwa nafasi ya kupigania viti hivyo mnamo tarehe nane mwezi wa nane mwaka huu."
}