GET /api/v0.1/hansard/entries/740606/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 740606,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/740606/?format=api",
"text_counter": 200,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "swala hili, tulikubaliana na wenzetu wa jinsia ya kiume kuwa tusipoweza kugawanya hii, igawanywe kwa asilimia kadhaa kila wakati kwa muda unaofaa. Lakini Mswada huu haukutaja hayo. Na kwa sababu hayakutajwa, siwezi kuyazungumzia kwa sababu Mswada ulioko mbele yetu unazungumzia kuwa baada ya miaka ishirini, tuwe tumefikisha thuluthi zile ambazo zinatakikana. Lakini tunavyoangalia na kuona ni kuwa bado katika muda ule wa miaka ishirini kutakuwa bado kuna tatizo. Kuna umuhimu wa sisi kuwa na sheria ambayo itatuwezesha kurekebisha tatizo hili ili Kipengele cha 27 kwenye kurasa zinazozungumzia haki za kibinadamu kiwezeshwe kufanyika haraka iwezekanavyo. Hili ni tatizo ambalo korti imefanya uamuzi kuwa tukutane na kusuluhisha jambo hili. Lakini wakati huu, Wabunge wengi wametoka kutafuta kura. Kila mtu anakitetea kiti chake pahali alipo. Itatuhitaji kufanya kazi ya ziada ili tuweze kupata idadi ya watu wanaotakikana. Kenya inaweza tu kusonga mbele vizuri kama tutakuwa na idadi ya akina mama ambayo inahitajika. Katiba ilijaribu kutupatia idadi lakini vile tumeona katika wakati wa uchaguzi wa mchujo, wananchi wenyewe hawakutaka kupatia nafasi wale akina mama waliochaguliwa kwenye maeneo ya ugatuzi kuwa Wabunge na kupata viti vile vingine. Ukiangalia Kipengele cha 100 kwenye Katiba yetu ya Kenya, kinazungumzia kuwe na makusudio ya kuangalia kuwa kina mama, walemavu na vile vile vijana wamehusishwa. Kipengele cha 100 kinazungumzia masuala mengi. Inatubidi tuangalie kurekebishwa kwa Katiba hii lakini vile vile tuangalie kama kuna uwezekano wa hicho Kipengele cha 100 kuwezeshwa ili tuweze kukitumia kupata idadi ya watu vile inavyotakikana. Kama ninavyosema, mimi kwa upande wangu nilikuwa nimeona kuwa ingekuwa rahisi kama asilimia hiyo ambayo inatakikana ifike ingeangaliwa kwa muda wa miaka kadhaa ili tufikishe idadi ya jinsia ya akina mama inavyotakikana hapa Bungeni. Kuna umuhimu wa sisi kuyazungumzia masuala haya, kupitisha sheria hii na kukubaliana. Hata viongozi wa vyama vyetu vilivyotuleta hapa, wote wamesema wazi hadharani kuwa kuna umuhimu wa kuhakikisha kuwa akina mama wanahusishwa kwenye Bunge letu la kitaifa na bunge la kaunti. Nitakomea hapo kwa kuwaomba wenzangu wote tuhusike tuweze kusaidiana na kuangalia njia ambayo swala hili linaweza kutekelezwa."
}