GET /api/v0.1/hansard/entries/744908/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 744908,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/744908/?format=api",
"text_counter": 431,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika. Kwanza, nachukua nafasi hii kumpatia kongole dadangu Mhe. Sabina Chege kwa kutupatia Mswada kama huu. Sisi kama viongozi akina mama 47, sababu moja ambayo kulitengezwa viti hivi ni kuwa tuweze kuhakikisha haki za akina mama na watoto zimeangaliwa. Katika Mswada huu, ametimiza jukumu lake kama kiongozi wa akina mama. Sote tunafahamu kwamba maziwa ya mama ni muhimu sana kwa mtoto mchanga kwa sababu yanapunguza maradhi mengi ambayo yangekuwa rahisi sana kumshika mtoto katika umri mdogo kama ule. Vile vile, tukizingatia watoto ambao wamezaliwa na maradhi ya kisasa ya ukimwi, madaktari wanahimiza sana mtoto yule anyonyeshwe kwa muda wa miezi sita bila kupatiwa chakula kingine chochote. Hivyo basi, ikiwa mzazi hatapata nafasi ya kumnyonyesha mtoto, itamlazimu ampatie chakula mbadala ama maziwa mbadala. Hivyo basi, atapunguza nafasi zake za kusaidika katika kujikinga na maradhi. Jambo la pili, Mswada huu umezungumzia kuwekwa kwa nafasi ambazo wazazi akina mama watatumia kunyonyesha watoto wao. Hili ni jambo muhimu sana, haswa tukizingatia The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}