GET /api/v0.1/hansard/entries/744911/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 744911,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/744911/?format=api",
"text_counter": 434,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "huwa kwao ni haba. Vile vile, huwa hawapati nafasi yoyote ya mapumziko katika siku nzima ambayo wako kazi. Kwa hivyo, Mswada huu utakopopitishwa, wale waajiri wa kibinasfi watahakikisha kwamba wamefuata sheria hii inavyotakikana. Kama ndugu yangu Tong’i alivyozungumza, kuna masuala katika Mswada huu ambayo yatakuwa magumu kwa waajiri. Pengine, katika kutengeneza ile nafasi na kuhakikisha kwamba taratibu zilizoko katika Mswada huu zimefuatwa, itakuwa ni vizuri waangalie mipango za zile nyakati ambazo mama yule anaweza kupatiwa ruhusa ya kurudi nyumbani kumnyonyesha mtoto kwa njia inayotakikana. Ikiwa hataweza, itambidi afuate sheria hii vile inavyosema. Vile vile, nakubaliana na mwenzangu aliyesema kwamba kunyonyesha ni njia mwafaka wa kupanga uzazi pasi na kutumia haya madawa ya kisasa ama hizi mbinu za kisasa za kupanga uzazi. Hivyo basi, iwapo Mswada huu utapita na utekelezwe, tutapunguza gharama nyingi na mambo mengi sana na yale matatizo yanayotokea kwa akina mama kutumia haya madawa ya kisasa ya kupanga uzazi. Swala lingine ambalo ningelizungumzia ni kwamba, lazima tuhamasishe akina mama. Wajulishwe ya kwamba Mswada huu umepitishwa wakati tutakaoupitisha ili wajue haki zao za kimsingi. Mama apate haki hii ya kuweza kumpatia mtoto mchanga pia haki yake ya kupata maziwa ya mama."
}