GET /api/v0.1/hansard/entries/744912/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 744912,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/744912/?format=api",
"text_counter": 435,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Swala hili ambalo Mheshimiwa amelitoa ni nzuri sana. Wakati wametengeneza zile nafasi, tusiweke na kusema: ―Tumeambiwa basi tufanye tu kwa njia ya kuonekana tumefanya. Lakini hatufanyi kwa njia ya sawa.‖ Tumeona akina mama wakikimbia kunyonyesha watoto chooni na kwenye jiko wakisema: ―Wacha nikimbie kunyonyesha mtoto hapa kwenye jiko. Nimeletewa mtoto na msichana wa kazi.‖ Sehemu kama zile haziwezi kumpatia mtoto nafasi nzuri na kumpa ile haki yake inayotakikana. Pia, nakubaliana ya kwamba dakika arobaine si nyingi. Ni za usawa kwa sababu kabla hujamnyonyesha mtoto, kuna mambo kadha wa kadha ambayo lazima yafanye. Nashukuru ya kwamba tumeambiwa kutakuwa na beseni ambalo mama ataweza kuosha matiti yake pale. Kutakuwa na jokofu ambayo tutakuwa tumehifadhi yale maziwa ili mtoto aweze kupewa. Kwa hivyo, hizi njia zote ambazo zimezungumziwa hapa zimezingatia mambo mengi sana ya kiafya na ya kuhakikisha ya kwamba huyo mtoto wakati amenyonyeshwa na mamake, atakuwa amepata ile kinga inayotakikana kwa mujibu wa madaktari wanavyozungumza."
}