GET /api/v0.1/hansard/entries/744913/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 744913,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/744913/?format=api",
"text_counter": 436,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Vile vile, ni jukumu la Serikali kushirikiana pamoja na taasisi za kiafya kuhakikisha hayo mambo mengine yasiyozungumziwa hapa kama vile kile chakula ama vitafunio yanatimizwa. Hii ni kwa ajili ya kuhakikisha kwamba watoto wataweza kukuwa kwa njia inayofaa kulingana na lisho bora. Najua kuna utaratibu wa mambo ya lisho bora unaofanywa kupitia zahanati zetu na Serikali. Kwa hivyo, kama kutakuwa na ushirikiano kama huo, hayo matatizo mengine yatakuwa si magumu kuyatatua kulingana na Mswada huu. Jinsi ulivyozungumza, mambo ya kuangalia mazingira vile yatakavyokuwa pale pahali ambapo pametengwa kwa mtoto kunyonyeshwa ni muhimu sana. Tusione tu ya kwamba tumeambiwa tuweke mahali na uchukue mahali pachafu. Lazima yawe ni mazingira ambayo hayatamfanya mtoto ama mama kupata maradhi yotote. Kwa hivyo, iwapo tutazingatia kabisa njia hizi na kufanya ushirikiano na vitengo vya kiserikali, taasisi za kiafya na pia vikundi vya akina mama kuhamasishwa kwa zile njia ambazo tutaweza The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}