GET /api/v0.1/hansard/entries/744914/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 744914,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/744914/?format=api",
"text_counter": 437,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "kuhakikisha kuwa Msaada kama huu umefanyika na kutekelezwa, Bunge hili litakuwa limeweka historia nzuri sana ya kuwafikiria watoto wachanga na akina mama na kuwapatia haki zao. Hakuna jambo nzuri kama mama kuwa na nafasi ya kumnyonyesha mtoto. Hiyo ndio njia ya kuwa yule mtoto anasoma mambo mengi kutoka kwa mama na anaweza kufahamiana na mamake kwa karibu sana, kwa sababu mtoto mchanga anasomeshwa na mama. Sisi akina mama huwa wakati tunawanyonyesha tunawazungumzia na kuwasemea. Wao pengine watacheka tu, lakini katika kule kucheka, ndio ya kwamba amesoma yale ambayo umemweleza na kumufahamisha. Kwa hivyo, ile njia ya kusoma kwa mtoto inaanzia mbali sana tangu akiwa mtoto mchanga mpaka akifika kuvunja ungo na kuendelea juu. Njia hii ya mama kunyonyesha ni mojawapo ya kuwafunza watoto wetu wachanga. Kwa hayo machache, nasema shukrani sana na kongole dada Sabina kwa kuleta Mswada huu. Asante."
}