GET /api/v0.1/hansard/entries/746933/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 746933,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/746933/?format=api",
"text_counter": 376,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Ngunjiri",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1179,
"legal_name": "Onesmas Kimani Ngunjiri",
"slug": "onesmas-kimani-ngunjiri"
},
"content": "Nashukuru sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Nasimama kuunga mkono Hoja hii. Nina hakika Wabunge wote tutaunga mkono Hoja hii kwa sababu inapendekeza utaratibu mwafaka. Maji ni uhai. Nina hakika wakati tuliamka asubuhi, hakuna mtu hakutumia maji. Kwa hivyo, maji ni kitu cha muhimu sana. Nakubaliana na wale ambao wamesema kuwa utaratibu wa maji lazima upangwe kwa njia nzuri. Najua tuna maji ya kutosha lakini mikakati ya kuweka maji pamoja sharti iwepo. Sharti wizara mbalimbali ziwekwe pamoja ili zitengeneze utaratibu kuhusu ukusanyaji na matumizi ya maji. Wananchi sharti waelewe kwamba nafasi na maeneo ya kujenga barabara ni wao wanapaswa kutupatia. Wasipotenga ardhi ya kutengenezea barabara, hali itakuwa ngumu. Maji ni mengi, hasa ya mvua. Tusipoyakusanya, tutazidi kuwa na shida ya maji. Maji yamekuweko, lakini hatukuweka mikakati ya kuiteka ili itusaidie kesho. Hili ni jambo tunalohitaji kuangazia kwa kina. Tunastahili kushikana sote ili tusaidie watu kwa njia nzuri itakayotusaidia kwa maisha yetu baadaye na ya watoto wetu. Maji inapotea kwa sababu ya kukosa mikakati na sheria. Hii inafanya tupoteze maji kwa wingi. Mvua imenyesha kwa muda mfupi sana na watu wameanza kulia kwamba maji imeharibu mashamba na mabonde mengine. Baada ya wiki mbili mvua ikiisha, tunaanza kulia kuna ukame. Hii ni kuonyesha ya kwamba hatujaweka mipangilio na mikakati vile inavyotakikana."
}