GET /api/v0.1/hansard/entries/749016/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 749016,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/749016/?format=api",
    "text_counter": 160,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Kipyegon",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1453,
        "legal_name": "Johana Ngeno Kipyegon",
        "slug": "johana-ngeno-kipyegon"
    },
    "content": "isiletwe hapa Bungeni. Leo nimefurahi kwa sababu Mheshimiwa Gumbo amewaasilisha Ripoti hii. Tunajua yeye anaaga hili Bunge kwa kuwa anatafuta kiti cha ugavana. Tunamtakia makuu na mazuri kwa sababu hajatuacha bila ya kuwasilisha Ripoti ambayo tumekuwa tukisubiri kwa muda mrefu. Masuala yaliyomo kwenye Ripoti hii hakika yameangamiza watoto wetu, wazazi na kila Mkenya. Watu wanapoongea juu ya sakata za ufisadi aina mbali mbali, mimi binafsi sikuzifahamu. Nilikuwa bado mtoto nilipokuwa nikisikia mengi kuhusu sakata mbalimbali. Ingawa hivyo, hii sakata ambayo imechunguzwa katika hii Ripoti nimeishuhudia. Nakumbuka wakati Mheshimiwa Alfred Keter, Mbunge kutoka Nandi Hills, alipoamsha haya maneno. Wakati huo, bwana mmoja kwa jina la Kiplimo Rugut alikuwa amehamishwa kazi. Ilibainika kwamba kulikuwa na jambo na sauti zingenyamazishwa. Baadaye, mtu alileta hapa ombi la kumtoa Waiguru kazini. Watu walipigiwa simu wakiombwa wasaidie kufuta majina yaliyotajwa. Inamaanisha kuna watu ndani ya Serikali ambao hawakuwa wanataka hili jambo lizungumziwe wala lipelelezwe, ili ijulikane ni akina nani waliiba pesa. Nakumbuka wakati rafiki zangu walikuwa wanapiga kelele, Naibu wa Rais alisema sisi ndio tunafaa kuwajibika. Alituambia tuachane nao. Baadaye, mambo yao yalipoumana mahali fulani, alibadilisha lugha akaanza kutuambia kuwa mtu hawezi kutembea kwa madaha na vishindo mbele yetu huku akiwa ameiba pesa za nchi ya Kenya. Kuhusu hii sakata ya ufisadi katika Huduma ya Vijana wa Taifa (NYS), tungependa kumwambia Rais wa Jamuhuri ya Kenya ambaye anatetea kiti cha urais jambo fulani. Sharti atuonyeshe kwamba chama chake cha Jubilee hakitaki ufisadi. Yeye angetuonyesha kupitia kura ambazo zimepigwa juzi za vyama - kwamba chama chake hakiwezi kuvumilia ufisadi. Nimesikia rafiki zangu wakiongea juu ya Waiguru. Wanasema kwamba siye pekee yake ambaye ameiba. Eti kunao wengi ambao, kama yeye, wanataka kuchaguliwa kwenye kura zijazo. Mmoja wa wale ametajwa ni Seneta wa Elgeyo Marakwet, Mheshimiwa Murkomen.Yeye ni wakili ambaye angetumia akili yake kujua kwamba kupora kutoka kwa raia ni hatia. Chama cha Jubilee hakijali kwamba hata Mheshimiwa Murkomen ametajwa katika hii sakata ya ufisadi. Yeye alipoulizwa haya mambo, alimtaja Mheshimiwa Gumbo, Mheshimiwa Rop na wanakamati wote wa Kamati ya Ukaguzi wa Fedha za Umma (PAC). Alisema kuwa walimtaka awape kitu kidogo ndiposa waondowe jina lake kwenye orodha ya waliyoshiriki katika ufisadi uliyotajwa. Ni jambo la ajabu kwamba Mheshimiwa Murkomen amepewa cheti cha kuwania kiti cha useneta ilihali, Serikali ya Jubilee inadai kuwa haitaki ufisadi nchini. Wao kumkubalia Waiguru na vile vile Murkomen ambaye alituibia kwa kutumia ofisi yake ya kazi, inamaanisha kwamba Jubilee iko ndani ya huo wizi. Nakumbuka pia jina la Mheshimiwa Duale lilitajwa. Hawa ni watu ambao juzi juzi walikuwa wanatembea hewani pasipo kulala. Nchi yao ilikuwa huko juu. Walikuwa wanaishi na kula huko juu. Kama kungekuwa na ndege ya kulala juu usiku, basi wangelala huko juu. Walilazimishwa kushuka kwa sababa hawengeweza kulala juu. Hawa ni watu waliozungukwa na pesa ya NYS ilhali, wamekuwa wakipiga mdomo. Duale alizunguka kila mahali huku akitusi watu kila kona. Alikuwa akitumia pesa za wizi. Inastaajabisha kwamba yungali kiongozi humu Bungeni. Ningependa nimwambie Mheshimiwa Rais Uhuru Kenyatta, Mungu tu ndiye atakusaidia urudi katika kiti cha urais. Akikubalia urudi, fagia nyumba yako maana ni chafu na wezi wamejaa kila kona. Ni kama nyumba iliyojaa panya kwa kuwa haina paka. Ukiingia kila kona, kuna panya mpaka hata ukileta paka moja, panya zote zitakusanyika na kuikula hiyo paka. Maneno haya ndiyo yako kwa Serikali hii ya Jubilee. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}