GET /api/v0.1/hansard/entries/752461/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 752461,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/752461/?format=api",
    "text_counter": 165,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Mhe. Spika, nashukuru kupata nafasi hii kutoa wasia wangu wakati nakunja jamvi kuagana na wenzangu - kuhusu Ripoti hii na kuhusu Bunge la Afrika mashariki. Si sahihi kwa hii Ripoti kunakili katika ukurasa wa 17 kuwa Chama cha ODM kilipeana majina matano. Mimi mwenyewe ndiye nilipeleka haya majina. Majina yalikuwa manne. Kwa hivyo, hii Ripoti imechangia kwa undani sana kuleta mambo ambayo hayakuweko. Nashangaa kwa nini kama tuna wafanyikazi ambao wanatakiwa kunakili kwa ufasaha yale ambayo yametokea, kuletea Bunge maandishi ambayo si sahihi. Kipengele cha 6(a)(i) kinasema kuwa kila chama kiko na nafasi ya kuleta watu ambao wamepatiwa. Hivi sasa, tunataka tukigeuze ili tutimize matakwa ya wenzetu. Huwezi kugeuza sheria ili kutimiza yale unataka. Wazungu wanasema: “ The law cannot be appliedretrospectively.” Mheshimiwa Spika, ni wasia wangu tusikimbizane na muda. Kama itabidi, basi tungoje Hoja hii ipitishwe na Bunge la kumi na mbili. Hatuwezi kuketi hapa kusema eti lazima chama kilete majina kadha wa kadha. Nakubalina na Bunge jinsi ilivyopitisha jambo hili kwa kauli moja. Kwa minajili hiyo, chama cha Orange Democratic Movement (ODM) kimeleta majina matatu, nacho chama cha Wiper jina moja kwa mujibu wa sheria. Sudan Kusini nayo imekumbwa na tatizo ikabidi iende mahakamani. Nakubali kwamba nasi pia tumechangia vilivyo kukwama kwa shughuli katika Bunge la Afrika Mashariki. Ingawa hivyo, iwapo tungekuwa na nia moja sisi sote, basi hili janga halingetupata. Kilichopo ni kwamba sote tuliangalia sheria tofauti tofauti, tukazinakili tofauti tofuati. Chama cha Jubilee kikaleta majina kulingana na vile kilivyofikiria. Chama cha CORD nacho kikaleta majina jinsi kilivyotafsiri hiyo sheria. Ndiyo maana Mheshimiwa ole Metito anapendekeza kwamba tugeuze hicho kipengele ili kusiwe na tafsiri mbali mbali za hiyo sheria. Lakini huwezi kugeuza hiyo sheria sasa hivi kwa sababu ya haya majina tuliyoorodhesha!"
}