GET /api/v0.1/hansard/entries/752582/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 752582,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/752582/?format=api",
"text_counter": 286,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwanyoha",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2308,
"legal_name": "Hassan Mohamed Mwanyoha",
"slug": "hassan-mohamed-mwanyoha"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Spika. Ninakushukuru kwa kunipatia nafasi hii ili niongee machache. Ninawashukuru watu wa Matuga kwa kunipatia kipindi cha miaka minne na miezi miwili kuwatumikia. Ni imani yangu kwamba kutokana na kazi ilivyofanyika, tutakuwa pamoja tena hapa mimi na wewe kwani nina imani pia kwamba wewe utarudi na kumbuka kwamba kura yangu ni yako. Kwa hivyo tutakuwa pamoja hapa mara tu baada ya uchaguzi. Mhe. Spika, safari yangu ya kuja Bunge hili ilikuwa ndefu sana. Ilianza mwaka wa 2002 nikipelekwa huku na huku, nikiibiwa hapa na pale na nikienda kortini na hakimu akiniambia kwamba mjadala wangu ulikuwa mzuri na kamili lakini mwisho uamuzi wake ni kwamba kila mtu arudi afanye kazi yake. Muda huo, kazi yangu ilikuwa ni kukanyaga lami kwa sababu mwenzangu alikuwa Mbunge. Sikujua kwa nini mahakimu hao walitoa uamuzi huo. Mhe. Spika, ninataka nikariri maneno yangu niliyoyazungumza miezi minne iliyopita. Nilikwambia kwamba wewe ni dume kwa sababu kazi uliyoifanya ilikuwa kazi ngumu. Bunge hili katika Afrika nzima ndilo Bunge ambalo lilikuwa na madume na kama ungalikuwa kiongozi legelege, wewe hata ungalijiuzulu kwa sababu Bunge hili lilikuwa na watu wakali mno lakini uliwahimili na ukatuongoza mpaka wakati huu. Kongole kwa shughuli zako nzuri. Mwisho, ninawaombea wenzangu wote ambao wamekata shauri kurudia viti vyao. Ninaomba wafaulu. Nilipoingia hapa nilikuwa na hofu huenda watu wakapigana ndani ya nyumba hii. Kumbe ilikuwa hali ya kujuana vizuri na kutengeneza urafiki. Hivi sasa nina marafiki mia tatu na arubaini na nane ndani ya nyumba hii baada ya kukaa kwa huo muda wote. Mheshimiwa Spika, ninataka nikushukuru kwa kazi nzuri uliyoifanya na Mungu atubariki sote."
}