GET /api/v0.1/hansard/entries/754214/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 754214,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/754214/?format=api",
"text_counter": 194,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Ahsante sana, Bi. Naibu Spika wa Muda. Hoja hii imekuja wakati unaofaa lakini ni lazima kwanza tuangalie chanzo cha matatizo haya. Alipokuwa Waziri wa Kilimo Makamu wa Rais William Ruto, wakulima katika eneo la Pwani walivuna chakula kingi mpaka wakakosa mahali pa kukihifadhi na kikaoza. Kuna shida katika Wizara ya Kilimo. Tunaomba Waziri wa Kilimo wa sasa aige mfano wa Mheshimiwa Ruto. Tunaomba asikae ndani ya ofisi bali aende mashambani akajionee na awasikize wananchi. Halmashauri ya nafaka nchini imejitwika majukumu yakuleta mbolea, ambayo si majukumu yake. Kama halmashauri hiyo imeshindwa kutuletea mbegu, italeta mbolea? Tumeipitisha Katiba ambayo imeanzisha serikali za majimbo. Sielewi ni kwa nini mpangilio wa ugavi wa mbegu ama mbolea umebaki katika Serikali Kuu. Inafaa kila kaunti inayofanya shughuli za kilimo ipelekewe pesa inunue mbolea na kuwapatia wakulima. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}