GET /api/v0.1/hansard/entries/754215/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 754215,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/754215/?format=api",
    "text_counter": 195,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "Mamlaka ya kununua mbegu yatakapopewa kaunti na taasisi iliyopendekezwa kuundwa, bodi ndogo katika kaunti zitapatiwa hayo mamlaka na tutaweza kupata mbegu na mbolea kwa wakati unaofaa. Wakati huo itakuwa rahasi kuwatambua wale ambao watakuwa wanazembea katika kazi zao, kinyume na hali ilivyo sasa, ambapo uzembe uko katika Serikali Kuu. Wakenya wanalia kwa sababu mbegu na mbolea haziwafikii kwa wakati unaofaa. Ninakumbuka kwamba katika miaka ya 90, kule kwetu Pwani kuliletwa mbegu iliyoitwa “Coast Composite”. Mbegu hiyo ilizaa ajabu lakini kulipoonekana kwamba Wapwani walianza kupata chakula, mbegu hiyo iliangamizwa. Sasa tunaletewa mbegu ndani ya mifuko. Tunaambiwa ndiyo mbegu inayofaa lakini tukipanda mahindi yanazaa yakiwa futi moja. Tutapata vipi chakula sisi Wapwani? Bi. Naibu Spika wa Muda, wakati umefika wa haki kutendeka kupitia kwa majimbo yetu. Nina imani kwamba Serikali hii itaweza kutilia maanani kwamba bila ya chakula hatuwezi kufika popote. Kilimo ni njia moja ya kuleta ajira. Kuanzisha kiwanda cha kutengeneza mbolea ni njia moja ya kuleta ajira. Nchi kama Israel inaweza kutengeneza mbolea yake. Unapoingia Mombasa na sehemu nyingine za Nairobi, unashindwa hata pa kupitia. Kunanuka uvundo. Uchafu umeenea kila mahali licha ya kwamba uchafu huo unaweza kugeuzwa na kufanywa mbolea. Tunaomba shirika lililopendekezwa liundwe lihakikishe kwamba katika kila eneo kutakuwa na kiwanda cha kutengeneza mbolea. Tukifanya hivyo, tutaweza kuisafisha miji yetu na kuwa na mazingira masafi. Tutakuwa tumeua ndege kumi kwa jiwe moja. Kwa hayo machache, ninaiunga mkono Hoja hii."
}