GET /api/v0.1/hansard/entries/755352/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 755352,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/755352/?format=api",
    "text_counter": 126,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Yusuf Hassan Abdi",
    "speaker_title": "The Member for Kamukunji",
    "speaker": {
        "id": 398,
        "legal_name": "Yusuf Hassan Abdi",
        "slug": "yusuf-hassan-abdi"
    },
    "content": "Nawasihi ndugu zetu wa Upinzani wasione kwamba Kenya ni ya vyama na mikoa. Kenya ni nchi moja na tunahitaji kuwa pamoja tushikane pamoja tuipeleke mbele. Mnapoenda kutafuta mzozano, mnaumiza uchumi wa nchi yetu. Mkienda kuzozana, mnaumiza umoja wa nchi yetu. Tupeleke Kenya yetu mbele na tujenge nchi yetu pamoja. Ikiwa mnataka kugeuza mambo, tuje hapa pamoja tuyageuze kidemokrasia na sio huko nje ambayo ni extra-parliamentary activities . Wawachie hao makereketo wakongwe wafanye hiyo kazi. Hawako Bungeni kwa sababu hawakuchaguliwa. Wao wakae huko na sisi tufanye kazi yetu tuendelee na hoja yetu na tuchague viongozi watakaoendesha kazi za Bunge, ili iendelee mbele bila kupoteza wakati."
}