GET /api/v0.1/hansard/entries/755356/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 755356,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/755356/?format=api",
    "text_counter": 130,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Kathuri Murungi",
    "speaker_title": "The Member for South Imenti",
    "speaker": {
        "id": 2802,
        "legal_name": "Kathuri Murungi",
        "slug": "kathuri-murungi"
    },
    "content": "Bila kupoteza wakati, Mhe. Mbadi alitoa hoja ya nidhamu na ukapeana mwongozo dhabiti ya kwamba hii Hoja itaendelea vizuri mpaka mwisho. Sidhani kuna haja ya hoja ya nidhamu tena kuuliza utoe uamuzi mwingine. Kwa hivyo, ningeomba tufanye hima kabisa tumalize hii Hoja iliyoletwa na Kiongozi wa Wengi Bungeni, ndio tuweze kuchagua hii Kamati. Nimeangalia haya majina yote manne na bila shaka nimeona wengine wamekuwa hapa kwa miaka mingi. Mhe. Kimunya alikuwa Waziri kitambo na kwa hivyo anaelewa kabisa ni kazi gani inastahili kufanywa katika Kamati hii. Kuna Mhe. Shadrack Mose na Mhe. Joyce Emanikor. Mhe. Joyce Emanikor tulikua naye kwenye kamati moja katika Bunge la 10. Yeye ni mbunge ambaye anaelewa kazi ya kamati hii. Mhe. Kawira Mwangaza, pamoja nami, tuliwania viti vya uwakilishi bungeni bila ya kupitia kwa vyama vya kisiasa. Tulijisimamia kama baba na mama. Namshukuru yeye pia kwa kuwa amepata wadhifa wakushikilia nafasi katika Bunge la 12."
}