GET /api/v0.1/hansard/entries/755357/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 755357,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/755357/?format=api",
"text_counter": 131,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kathuri Murungi",
"speaker_title": "The Member for South Imenti",
"speaker": {
"id": 2802,
"legal_name": "Kathuri Murungi",
"slug": "kathuri-murungi"
},
"content": "Mhe. Spika, wakati ulipoitisha kikao cha kuapishwa kwa wabunge, wenzetu walio wachache Bungeni hawakuamini kwamba hilo jukumu lingetekelezwa vizuri. Ulipoitisha kikao cha ufunguzi rasmi wa Bunge na Mhe. Rais, wao hawakuamini kwamba shughuli hiyo ingetekelezwa vizuri. Sasa wanakimbia hapa na pale, “helter skelter”, kwa sababu wameona kwamba Bunge na taasisi nyingine za umma nchini zinaendelea kufanya kazi, wawe Bungeni ama wasiwe. Nimefurahishwa na jinsi wote wanavyokimbia hapa na pale, na haswa Mhe. John Mbadi, ambaye huwa mgumu sana kwa mambo mengi. Leo nilimuona akimuomba Mhe. Spika ampe nafasi ili aweze kuyaleta Bungeni majina ya Wabunge kutoka mrengo wa Upinzani watakaohudumu kwenye kamati hii. Kwa hivyo, tutaendelea kuijadili Hoja hii. Watakapoleta majina yao, tutaongea kwa masaa mawili halafu tuifanyie mabadiliko Hoja hii ili tuyaongeza majina hayo. Kwa hivyo ninashukuru. Nikimalizia, nawashukuru wakazi wa South Imenti kwa kunipa nafasi ya kuwawakilisha tena katika Bunge la 12. Ninawahakikishia kwamba nitawafanyia kazi bila ya kuchoka mpaka miaka mitano iliyosalia ikamilike. Ahsante sana, Mheshimiwa Spika."
}