GET /api/v0.1/hansard/entries/755528/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 755528,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/755528/?format=api",
"text_counter": 120,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Asante, Mheshimiwa Spika kwa fursa hii. Ningependa kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu Muumba anayetoa cheo. Pia, ningependa kusema kongole kwako. Kuchaguliwa kwako kunaonyesha ishara kwamba chama cha Jubilee kipo, kinatawala na kitatawala. Kwa mara ya tatu, watu wa Bura wamenichagua kuwawakilisha katika Bunge hili. Sina la kuwalipa kwa sababu ya mapenzi yao. Nawashukuru na ningependa kutangaza kwao leo kuwa nawapenda na nitawahudumia kwa haki. Nimesikia Hotuba ya Rais na inanifundisha ujasiri. Leo ukitangaziwa kuwa umepoteza kiti cha Ubunge, wengi watapelekwa hospitali. Lakini Rais wa taifa alipoambiwa kuwa uchaguzi utarudiwa, alisema kuwa ana shaka na maamuzi hayo lakini atayaheshimu na yuko tayari kuenda uwanjani. Kama askari wake, mimi niko tayari kumpigia na kumwombea kura. Katika Hotuba yake, nilitarajia Rais agusie masuala ya ukame. Tunavyozungumza leo, maji ni nadra kupatikana katika sehemu kubwa ya Bura, haswa sehemu ya Bangale, Hirimani na Bwoka. Iwapo Serikali haitasimama wima na kushughulikia jangwa la ukame na ukosefu wa maji Bura, sijui tutapiga kura namna gani. Nilikuwa natarajia nisikie masuala ya deni ya wakulima wa Bura. Ni vipi mzigo wa deni utaondolewa ili wakulima wote wa Kenya, haswa wakulima wa Bura, waweze kujimudu kimaisha? Mambo haya hayakusikika katika Hotuba yake Rais. Hayakusikika kwa sababu wana- NASA wameenda kortini na wakavuruga ushindi wa Wakenya. Leo Rais anajiwekea mipaka. Hawezi akaguza sehemu nyingine. Vijana wananiambia kuwa kuna demokrasia mpya katika nchi ya Kenya wanaita “Demokrasia Maraga”. Demokrasia si mchakato; demokrasia ni hesabu. Hesabu haidanganyi. Nilikuwa na maombi dhidi yangu katika mwaka wa 1997 kwa mara ya kwanza na nimekuwa na maombi dhidi yangu kwa mfululizo mpaka mara hii. Mara hii kwa bahati nzuri, sina ombi dhidi yangu. Nafikiri wamesahau. Yale yaliyopelekwa kortini yananishangaza kama yanatosha kuharamisha uchaguzi wa Rais. Yananishangaza kwa sababu hawakuomba kurejelewa kwa hesabu. Wanasema mchakato, si mpiga kura. Upigaji wa kura ni haki ya mwananchi ambayo haistahili kunyakuliwa au kunyang’anywa na mtu yeyote - uwe jaji ama nani. Nashangazwa nikiambiwa kuwa hesabu ya kura milioni nane si shida. Shida ilikuwa katika Fomu 34A, 34B na The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}