GET /api/v0.1/hansard/entries/755584/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 755584,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/755584/?format=api",
    "text_counter": 176,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Marwa Kemero Maisori Kitayama",
    "speaker_title": "The Member for Kuria East",
    "speaker": {
        "id": 13394,
        "legal_name": "Marwa Kemero Maisori Kitayama",
        "slug": "marwa-kemero-maisori-kitayama"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika. Kwanza ningependa kumshukuru Mungu kwa ajili ya nafasi ambayo amenipa kuwakilisha watu wangu wa eneo Bunge la Kuria East. Hongera nyote ambao mmechaguliwa kuwakilisha watu kutoka maeneo ambayo mmetoka. Mhe Spika, hongera kwa ajili ya kuchaguliwa vilevile. Vilevile nachukua nafasi hii kushukuru Mungu kwa sababu ya Rais wetu. Tabia ambayo ameonyesha, utu ambao ameonyesha tangia mambo haya yamefanyika imetutia sisi moyo sana. Kulingana na Hotuba ambayo Rais alitoa jana, kipengele kile ambacho alizungumzia kuhusu mambo ya ugatuzi… Sisi ambao tunatoka sehemu ya Kuria na maeneo mengine yenye makabila madogo madogo, jambo hili la ugatuzi... Aliposema kwamba Bunge la Kumi lilifanya kazi nzuri kuzalisha Katiba mpya, Bunge la Kumi na Moja likafanya kazi nzuri ya kulea Katiba hii, mahali ambapo alitaja kwamba Bunge hili litaendeleze demokrasia yetu, hapo ndipo ningependa kulenga. Ingependeza sana kwamba Bunge hili tuangazie zaidi jinsi ambavyo tutafanya ugatuzi endelezi. Jinsi ilivyo sasa ni kwamba gatuzi nyingi zimeshikwa mateka na wale ambao tumewapa mamlaka ya kuendeleza ugatuzi. Magavana wengi, sisi wote tunajua, baada ya kupata mamlaka wameachia palepale. Hakuna ugatuzi unaendelea zaidi ya makao makuu. Hotuba ya Rais kwamba Bunge hili liendeleze utaratibu wa kupanua nafasi ambayo inajumuisha hata jamii zile ambazo ziko katika maeneo ambayo hayawezi kupata haki kwa sababu ya uchache kama vile Wateso, Wakuria na sehemu zingine kama Mlima Elgon, kuna haja ya Katiba hii, nikitumia maneno ya Rais, “ we should revisit .” Kuna mambo ya kurejelea. Wakati ambapo tulikuwa tunajadili Katiba hii, tulisema kwamba asilimia themanini ni nzuri, lakini asilimia ishirini ina matatizo. Katika hiyo asilimia ishirini, napendekeza kwamba Bunge hili tupate nafasi nzuri ya kuendeleza ugatuzi huu ili hiyo asilimia iliyobaki, ikiwemo kuweka sheria ambazo zitahakikisha kwamba kuna kuendelea kugatua hata zaidi ili watu ambao wanatoka katika jamii ndogo wapate haki yao. Ningependa kutoa mfano. Juzi katika uchaguzi wa Spika kule Migori County, Mkuria alipata kiti halafu akapigwa akanyang’anywa na hakuwa na mtu wa kumtetea. Jambo kama hili litakaporuhusiwa kuendelea, basi itakuwa hakuna haki tutapata sisi ambao tunatoka katika jamii ndogo. Kwa hivyo, Hotuba hii ya Rais, haswa ikilenga suala hili la ugatuzi, ilinisisimua sana na nikajua kwamba hili Bunge litawaokoa wale ambao sehemu zao hazisikiki kwa sababu ya jinsi ambavyo mfumo huu wa ugatuzi ulivyo. Nisingependa kusema maneno mengi kwa sababu najua wengine watachangia. Ni vizuri kwamba tumepata nafasi hii ya kuwaakilisha watu wetu. Asanteni sana watu wa Kuria East kwa kunichagua. Naamini kwamba nitawatumukieni kwa njia iliyo bora. Naomba Mwenyezi Mungu atusaidie. Asanteni kwa kunisikiza. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}