GET /api/v0.1/hansard/entries/755599/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 755599,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/755599/?format=api",
    "text_counter": 191,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "The Woman Representative for Kajiado County",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "(Hon. (Ms.) Janet Marania Teyiaa): Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Mimi ni Mbuge wa Kaunti ya Kajiado. Kwanza ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa nafasi hii ya kurudi Bungeni nikiwa nimechaguliwa. Pili, nawapongeza waheshimiwa wenzangu kwa kurudi kwenye Bunge la 12. Nawashukuru wananchi wa Kaunti ya Kajiado kwa kunichagua niwawakilishe Bungeni nikiwa mama mlemavu. Wamevunja rekodi na kuonyesha kwamba yote yanawezekana. Nikizingatia Hotuba ya Rais, ninampongeza kwa sababu ameonyesha kwamba yeye ni mtu mnyenyekevu na mwenye amani. Namshukuru kwa kuwa aliweza kunitambua nikiwa mmoja wa akina mama waliowania kiti hiki kupitia chama cha Jubilee. Ningependa kumshukuru Rais kwa sababu alinitambua kama mmoja wa akina mama ambao walisimama katika chama chake. Yeye ameniheshimu. Ametambua uongozi wa akina mama na kwa hivyo akina mama wengi wamechaguliwa katika Bunge la Kumi na Mbili. Hali imekuwa hiyo kwa vijana na wenzetu wanaoishi na ulemavu ambao kwa miaka mingi hawajapata kuwakilishwa Bungeni. Kwa hivyo, hali imebadilika."
}