GET /api/v0.1/hansard/entries/755605/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 755605,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/755605/?format=api",
    "text_counter": 197,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Vincent Tuwei Kipkurui",
    "speaker_title": "The Member for Mosop",
    "speaker": {
        "id": 13436,
        "legal_name": "Vincent Kipkurui Tuwei",
        "slug": "vincent-kipkurui-tuwei"
    },
    "content": "Nampongeza Rais kwa yale yote ambayo alisema katika Hotuba yake. Alisema kwamba sisi sote lazima tuwajibike kulinda na kudumisha Katiba. Sisi sote kama Wabunge, wao kama viongozi wakuu na idara ya mahakama sharti tuwajibike. Katiba yetu inahitaji kwamba mtu yeyote ambaye ana wajibu lazima azingatie mawazo na nia ya mwananchi. Madaraka haya yote ambayo tumevishwa ni kwa sababu ya mwanachi. Ukiwa Jaji Mkuu, Jaji, Rais, Mbunge, Seneta ama mwakilishi wa kaunti, wajibu na haki ni kwa mwananchi mwenyewe. Huyu ndiye amepewa haki zote kikatiba kwa sababu ni msingi wa nchi hii."
}