GET /api/v0.1/hansard/entries/755606/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 755606,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/755606/?format=api",
"text_counter": 198,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Vincent Tuwei Kipkurui",
"speaker_title": "The Member for Mosop",
"speaker": {
"id": 13436,
"legal_name": "Vincent Kipkurui Tuwei",
"slug": "vincent-kipkurui-tuwei"
},
"content": "Nashukuru kwamba sisi sote ambao tumechaguliwa hapa kama Wabunge ni viongozi tuliyochanganyika wazee, vijana, akina mama na walio na usumbufu fulani wa kimaumbile. Hii inamaanisha kwamba tuko hapa sote kisawa. Tuko hapa kwa sababu ya mwananchi na nchi yetu ya Kenya. Uchanguzi wa Rais ndiyo tatizo kwetu sasa. Suala litakuja mbele yetu Wabunge ili tujadili sheria ambayo inahusiana na uchaguzi. Mwananchi atakapo piga kura, basi uamuzi wake uheshimike. Isiwe kwamba mtu binafsi aliye na madaraka anatumia nafasi yake kuiletea nchi hii hasara. Pesa zote ambazo zitatumika katika uchaguzi wa tarehe 17 Oktoba ni za Wakenya."
}