GET /api/v0.1/hansard/entries/755612/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 755612,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/755612/?format=api",
    "text_counter": 204,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "The Woman Representative for Tana River County",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kutokana na hiyo Hotuba ya Rais ya jana hata mimi nataka kurudia alichosema Mhe. Ali Wario. Kuna mambo tuliyoahidiwa hata nilitarajia pengine angeyataja lakini sikuyasikia. Mimi nitarudia jambo la ukame. Sisi tuko na mto lakini umekauka. Wananchi wengi saa hii wanakufa kutokana na njaa na kiu. Hata niliona jambo la kusitikisha. Kwangu ni Madogo. Ninaposafiri kuja Nairobi, sehemu ya Banga ninawapata watoto wadogo wakiwa na chupa ndogo ndogo wakiomba maji njiani. Wanaomba watu ambao hawajui maji ya kunywa. Wale watoto wako katika hatari kwa sababu wanaweza kutiliwa madawa ya kulevya kwenye yale maji, kwa sababu huwezi ukajua adui wako ni nani. Mimi bado naomba na kutilia mkazo ili Rais atakapokaa akipanga mambo yake asisahau wananchi wa Tana River. Tuko na shida na tunahitaji maji tena kwa haraka iwezekanavyo."
}