GET /api/v0.1/hansard/entries/755657/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 755657,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/755657/?format=api",
    "text_counter": 249,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "The Woman Representative for Taita Taveta County",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "(Hon. (Ms.) Lydia Haika Mnene Mizighi): Ahsante sana, Bw. Naibu Spika. Ninaitwa Haika Mizighi kutoka Taita Taveta. Ninatangulia kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipatia nafasi ya kuwa hapa siku ya leo. Pili, wacha niwashukuru wananchi wote wa Taita Taveta County kwa kunipatia kura zao kwa wingi, kwa kuniwezesha kuwa mwakilishi wa akina mama katika Bunge hili la kitaifa nikiwa katika chama cha Jubilee. Hili si jambo la kawaida kule kwetu Taita Taveta, lakini wananchi waliniamini na wakanipatia fursa hii. Ninasema ahsanteni sana na mimi niko hapa kuwawakilisha bila uoga. Naungana na wananchi wengine, naungana pia na wenzangu hapa Bungeni kulijadili suala hili, ambalo ni Hotuba ya Rais wetu iliyosomwa hapo jana na yeye mwenyewe. Ninaungana na akina mama wenzangu wengi. Kwa kweli tumefurahi sana. Tunamshukuru Rais wetu kwa kuwa ametutambua sisi kama akina mama na uongozi. Ametambua juhudi zetu nyingi ambazo tumefanya na bidii tuliofanya kwa ajili ya kuweza kupata nafasi hizi za uongozi. Tunasema ahsante sana kwa Rais wetu. Natumai akina mama wote wa Kenya wameliona hilo. Tunapoelekea kwenya uchaguzi tarehe 17, wanamjua rais ambaye anasimama na akina mama, na ambaye anawatambua na kuwaheshimu akina mama kama viongozi. Jambo lingine pia ni kumpongeza sana Rais wetu kwa kuwa mstaarabu. Jana, alipokuwa akitoa Hotuba yake Bungeni, hakuchukua nafasi hiyo kuuza sera zake bali alituomba tuendelee na kazi na akasisitiza umuhimu wa kudumisha amani nchini Kenya. Kwa sababu hiyo, pia ninampongeza sana. Sisi tunasema tuko pamoja na yeye. Hata tarehe 17 tutasimama nayeye. Ahsante sana."
}