GET /api/v0.1/hansard/entries/755707/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 755707,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/755707/?format=api",
    "text_counter": 299,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "The Woman Representative for Lamu County",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "(Hon. (Ms.) Ruweida Mohamed Obo): Asante Mhe. Spika. Naitwa Ruweida, mwakilishi wa Kaunti ya Lamu. Ningependa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa nafasi hii. Pia nawashukuru wakaazi wa Lamu County kwa kunipa hii nafasi. Nitawahudumia kwa uadilifi, uwazi na ukakamavu. Kwa Hotuba ya Rais, ilinikumbusha 2013 wakati wa kesi ya mwakilishi mwanamke maana ule uamuzi uko tofauti na huu wa urais. Uamuzi ule nikijaribu kulinganisha na vile jaji alisema ni tofauti sana. Ule uamuzi wa 2013 kwa kesi yetu ulisema, “ The IEBC official hasbreached Article 83 of the Constitution by not signing Form 36 but the process at the very endwas validated by the gazettement .” Kwa hivyo sisi tuliambiwa tulipwe na IEBC Kshs1.5 milioni na mwenzangu akaendelea kuwa mwakilishi wa akina mama Bungeni. Uamuzi wa Mahakama ya Juu umekuwa tofauti sana. Hata hivyo, kwa vile Mhe. Rais anauhesimu uamuzi huo, nasi pia hatuna budi kuuhesimu. Tumehuzunishwa na Hotuba yake, hata hivyo tunamwambia Rais asihuzunike, hawa waheshimiwa ni wengi. Tuko na familia, marafiki na wafuasi wetu. Namba ishaonyesha, tutashuka mashinani, tumtafutie kura. Sina mengi, ninapongeza uongozi wa Bunge, ahsanteni. Mimi ni Mbajuni na ningependa nipendelewe kama Mbunge anayetoka katika jamii iliyotengwa. Mbajuni mwingine ni Mhe. Sharif kutoka Kaunti ya Lamu. Tuko watatu tu. Ningependa mtuangalie vyema. Ahsante, Mhe. Naibu Spika."
}