GET /api/v0.1/hansard/entries/755971/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 755971,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/755971/?format=api",
    "text_counter": 20,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Simon Ng’ang’a King’ara",
    "speaker_title": "The Member for Ruiru",
    "speaker": {
        "id": 13468,
        "legal_name": "Simon Nganga Kingara",
        "slug": "simon-nganga-kingara-2"
    },
    "content": " Ahsante sana Mhe. Naibu Spika. Mimi ninatoka Eneo Bunge la Ruiru katika Kaunti ya Kiambu. Eneo hili ni moja kati ya maeneo Bunge makubwa humu nchini na lina idadi ya watu 160,000. Ningependa kuwashukuru watu wa Ruiru ambao walinichagua na kunipigia kura zaidi ya 108,000. Nawapa shukrani kubwa watu wa Ruiru kwa kunipatia fursa hii ya kuwawakilisha hapa Bungeni. Sitasahau kurudisha shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa kutupatia ujasiri wa kuchagua Spika Mhe. Muturi na Naibu Spika. Mlihudumia Bunge muhula uliopita na tukaona ujasiri wenu na vilevile tukawachagua. Kwa sisi Wabunge, ni shukrani kwa wananchi wa Kenya kutupatia mwanya wa kuwawakilisha. Pia, ni shukrani kuu kwa Wabunge wote kwa kuchaguliwa katika maeneo yao. Hii inaonyesha wima wa Wakenya kwetu tuliochaguliwa. Nikiguzia kidogo kuhusu Hotuba ya Rais tumpendaye Uhuru Kenyatta, alianza na jambo la busara sana. Wakati alichukua kipasa sauti, neno lake la kwanza lilikuwa kuhimiza Wabunge kujua walichaguliwa kuhudumia Wakenya. Hilo ni jambo la uzito zaidi. Vilevile hakusahau kuwaambia Wakenya macho yote yamewaangalia viongozi wote waliochaguliwa kuleta amani na uwiano katika Kenya yetu tuipendayo. Hilo ni jambo la uzito kwa vile ukiangalia maeneo mengi katika Afrika, uongozi, usalama na maendeleo zimezorota. Lakini ukiiangalia Kenya, kiongozi wetu tumpendaye Uhuru Kenyatta ameiga mwigo mwema na ikawa kama kitabu cha The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}