GET /api/v0.1/hansard/entries/755972/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 755972,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/755972/?format=api",
"text_counter": 21,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Simon Ng’ang’a King’ara",
"speaker_title": "The Member for Ruiru",
"speaker": {
"id": 13468,
"legal_name": "Simon Nganga Kingara",
"slug": "simon-nganga-kingara-2"
},
"content": "kusoma wakati tunaendeleza maendeleo yetu. La muhimu, alisema hata kama kuna vurugu na joto kali la kisiasa, atasimama kidete kuona sisi viongozu tumetimiza majukumu yetu bila wasiwasi wowote ule. Na kama kiongozi wetu amesema hakuna wasiwasi, sisi ni akina nani kuwa na wasiwasi? Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kama kiongozi wetu hana wasiwasi. Sisi tuko wengi.Yeye ako peke yake na amesimama na uzito wa kuonyesha Kenya itakuwa na amani hata kama vipande vingine vimekaa vile wamekaa. La muhimu ni kuhimiza wote ambao wamechaguliwa kuja Bungeni ili tutimize yale ambayo tulichaguliwa kutimiza. Ni aibu kidogo wakati mtu ambaye amechaguliwa anakuja pale, anajaza karatasi, anaweka sahihi, anatoka nje na anangojea malipo kutoka kwa Wanjiku. Atakuwa amekosea Wanjiku na amejikosea mwenyewe kama Mkenya. Hilo ni ombi langu. Vile hakuna mtoto katika Bunge hili, tutumie utu wetu ule tumepewa na Mwenyezi Mungu na tusimame kuonyesha sisi ndio kielelezo chema cha maendeleo na haki katika Kenya yetu tuipendayo. Hayo yote hayatatimika kama hatutafanya hayo kwa matendo na sio kwa fikira tu. Mengi yamesemwa kuhusu maendeleo yetu. Katika eneo la Ruiru tuko na shida nyingi sana. Wenyeji wa Ruiru wanajua hivyo. Nimesimama hapa nikiwawakilisha na kuwahakikishia kuwa kutokana na uongozi mwema wa Uhuru Kenyatta, yale yote mnafikiria tunatakiwa kutenda tutayatenda. Nikitamatisha, ninaomba wale tuko hapa tuendelee kujuana ndio tufanye kazi kama ndugu na dada. Asanteni."
}