GET /api/v0.1/hansard/entries/756006/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 756006,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/756006/?format=api",
"text_counter": 55,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mohamed Ali",
"speaker_title": "The Member for Nyali",
"speaker": {
"id": 13398,
"legal_name": "Amin Deddy Mohamed Ali",
"slug": "amin-deddy-mohamed-ali"
},
"content": "kuwapongeza na kuwashukuru wana Nyali kwa kuamua kwenda kinyume na itikadi na siasa chafu za pesa, vyama na ukabila na badala yake kunichagua mimi kama mgombea huru katika eneo Bunge la Nyali. Nawapongeza pia Wakenya wote waliojitolea na kuchangia katika mkoba wangu wa Kampeni pamoja na ushauri walionipa. Sina la kuwapa ila nawaahidi kuwa nitazidi kuwapigania na kuwakilisha sauti zao katika Bunge la 12. Kwa ufupi, nasema Mungu awabariki wote kwa kuamini kuwa hakuna lisilowezekana mbele ya macho ya Mungu. Fauka na hayo, naomba hili Bunge la 12 liwe kielelezo na tofauti kabisa na Bunge za hapo awali kwa kujadili na kupasisha Miswada itakayo wakinga Wakenya dhidi ya udhalimu, ukiukaji wa haki za binadamu, ufisadi na mambo mengine ya kuchukiza. Mhe. Naibu Spika, mengi yalitajwa wakati wa Hotuba ya Rais, huku kukiwa na matumaini ya mambo kuwa sawa katika siku za usoni. Nchi inayoongozwa na demokrasia hufanya mambo yake kidemokrasia. Nchi inayoongozwa na demokrasia ya kijambazi hubaka demokrasia ya wananchi wa taifa hilo na kuwakandamiza. Ni matumaini yangu kuwa sote tutakuwa mamoja pasi na misingi ya dini, kabila, rangi au vyama kuilinda Katiba na taifa letu zuri. Letu kuu kama viongozi waliochaguliwa na Wakenya ni kuhakikisha kuwa safari hii hatutazalisha tena umaskini. Tuhakikisheni kuwa, kupitia sura hizi ninazoziona Bungeni – sura za Wabunge, maprofesa, wanahabari, madaktari, wahandisi, miongoni mwa wengine wengi – tutashikamana na kujenga Kenya kwa kutumia taaluma zetu na wala sio kuwa vibaraka wa kuabudu miungu binadamu. Kwa ufupi, tusikubali akili ndogo kutawala akili kubwa."
}