GET /api/v0.1/hansard/entries/756010/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 756010,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/756010/?format=api",
    "text_counter": 59,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mohamed Ali",
    "speaker_title": "The Member for Nyali",
    "speaker": {
        "id": 13398,
        "legal_name": "Amin Deddy Mohamed Ali",
        "slug": "amin-deddy-mohamed-ali"
    },
    "content": "Hakika sisi Wapwani tumeathirika pakubwa na watu wachache wanaojipiga kifua na kujiona kama miungu midogo huku wakiangamiza kizazi chetu. Safari hii tunaujumbe kwa walanguzi wa dawa za kulevya Pwani. Tunasema kama noma, naiwe noma . Wakenya wote ni mashahidi kwamba vijana wetu wengi wameendelea kudhoofisha afya zao kutokana na matumiza ya dawa za kulevya. Dawa za kulevya ni hatari sana kwa usalama wa ustawi wa taifa letu. Vita hivi ni vita vikubwa dhidi ya uagizaji, uzalishaji, usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya. Sote tunapaswa kuunga mkono jitihada hizi. Nikimalizia, nihitimishe hotuba yangu kwa kuombea waheshimiwa Wabunge-wenza, pamoja na Wakenya wote waliotutuma katika Bunge hili kama watumishi na wala si waheshimiwa, Mwenyezi Mungu atujalie sote nasiha njema katika kipindi chote tutakachokuwa mashinani kuwatumikia Wakenya waliotuchagua kwa kuchukua maoni yao na kuwawakilisha ipasavyo katika hili Bunge la 12. Mungu ibariki Kenya."
}