GET /api/v0.1/hansard/entries/756058/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 756058,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/756058/?format=api",
"text_counter": 107,
"type": "speech",
"speaker_name": "The Woman Representative for Nakuru County",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Nampongeza Rais kwa Hotuba yake. Ni Hotuba ambayo itaboresha nchi yetu ya Kenya na itawaleta wananchi wote pamoja. Ni Hotuba ambayo imezingatia sana amani katika nchi yetu. Najivunia sana Rais wetu pamoja na naibu wake. Ni viongozi jasiri. Wametuunganisha pamoja sisi wananchi wa Kenya tangu mwaka wa 2013 hadi leo. Kuna sehemu nyingi humu nchini ambazo hazikuwa na stima. Kwa kusema kweli, ni wapi duniani utapata Rais na naibu wake wakisisitiza kwamba umeme ufikishwe hadi kwenye nyumba zenye paa ya nyasi? Hizo ni nyumba za watu ambao hali yao ya maisha iko chini sana. Isitoshe, barabara pia zimejengwa. Ni wapi humu duniani utapata Rais ambaye anawaza kuhusu akina mama maskini? Tunajua kwamba kumekuwepo na tatizo la wanafunzi wasioweza kumaliza kulipa karo ya shule na kunyimwa vyeti vya shule. Rais na naibu wake waliamuru kwamba wanafunzi wote wapewe vyeti vyao. Aidha, walifutilia mbali ada ya mitihani."
}