GET /api/v0.1/hansard/entries/756110/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 756110,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/756110/?format=api",
"text_counter": 159,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Amin Deddy Mohammed Ali",
"speaker_title": "The Member for Laikipia East",
"speaker": {
"id": 13398,
"legal_name": "Amin Deddy Mohamed Ali",
"slug": "amin-deddy-mohamed-ali"
},
"content": " Ahsante sana Mhe. Naibu Spika. Ninawakilisha Eneo Bunge la Laikipia Kusini. Nimesimama kwa heshima zote na unyenyekevu kumushukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipatia nafasi ya utumishi. Ningependa kuwahakikishia ya kwamba nitawawakilisha kikamilifu. Majukumu ambayo wametupatia tunaamini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, tutayatekeleza kikamilifu. Mambo ambayo yako mbele yetu si rahisi. Tunajua kuna shida kwetu kutoka mahali panaitwa Wiyumire, Solio mpaka Umande. Tunajua akina mama walituchagua bila ubaguzi wakijua ya kwamba mizigo ambayo wamekuwa wakibeba kwa miaka yote, na changamoto ambazo ziko pale, tutaweza kuwarahisishia. Ningependa kumpongeza sana Rais kwa sababu aliongea kuhusu mambo ya ugatuzi na kupiga siasa kama mtu mzima. Alituelezea vizuri kwamba siasa ni mchezo wa siku moja na baada ya hapo maisha yataendelea kama kawaida. Ninawaomba Wabunge wenzetu wa mrengo wa NASA waje Bungeni tushiriki katika Miswada na mijadala ya kujenga nchi na kupeleka nchi mbele. Tunakemea pepo ambayo ni ya fitina, uchochezi na ukabila. Mimi nikisimama hapa, ninasimama kwa heshima zote kama mtu ambaye ametoka katika jamii ya wachache. Nimechaguliwa Laikipia, mahali ambapo watu wa kabila langu si wengi. Ningependa kuwaeleza watu wetu kutoka North Eastern waangalie na wafuate Jubilee kikamilifu. Mhehsimiwa Rais ametupatia nafasi ya utumishi na tuko hapa kutetaea Serikali ya Uhuru Muigai Kenyatta. Wakati wote tunaamini kwamba uongozi unatoka kwa Mwenyezi Mungu. Hata kwa lugha yetu ya nyumbani tunasema “ Utongoria umaga kwi Ngai”, tukimaanisha kwamba Mwenyezi Mungu anapeana uongozi kwa sababau zake. Tunaamini kwamba Hakuna lisilowezekana. Akina mama wamekuwa wakibeba mitungi kwa miaka mingi. Wao ndio waliotuzaa, wakatulea na kutuelimisha. Tuliomba nafasi ya kuja hapa ili tuwaondolee hiyo mitungi migongoni mwao. Itawezekana kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu. Mhe. Raila alisema kinaganaga kwamba yeye bado ako katika usukani, na nchi ya Kenya haina pengo la uongozi. Ameonyesha dunia nzima siasa ambazo zimekuwa zikiendelea; siasa za mgawanyiko. Lakini hapa Bungeni tuko pamoja. Idadi ya Wabunge kutoka mrengo wa Jubilee inatosha kuendesha shughuli za Bunge. Watu wa Laikipia Kusini, tuwekeni katika maombi. Tumekuja kufanya kazi, sio kupiga siasa za uchochezi na ukabila. Tumekuja kujenga nchi kwa sababu hata maandiko yanasema The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}