GET /api/v0.1/hansard/entries/756574/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 756574,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/756574/?format=api",
"text_counter": 98,
"type": "speech",
"speaker_name": "The Woman Representative for Laikipia County",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "(Hon. (Ms.) Catherine Wanjiku Waruguru): Ahsante sana Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii na pia kwa macho yako kunimulika. Ndiyo maana sichukulii jambo hilo kuwa la kawaida. Ningetaka kuchukua nafasi hii kuwashukuru watu wote wa Laikipia kwa sababu waliamua kwa sauti moja kumtuma mama kijana kwenye Bunge hili la Taifa. Nitawafanyia kazi. Ningependa kuchangia Hoja iliyo mbele yetu. Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Muigai Kenyatta, anatutaka sisi viongozi tushikane mikono pamoja ili tuelekeze taifa la Kenya kwenye barabara moja. Mhe. Spika haiwezekani eti sisi wanajubilee ambao tuko wengi hapa Bungeni tutazuiliwa kusonga mbele. Hatupaswi kuwapatia nafasi kubwa wenzetu katika Upinzani, ilhali tunayo Miswada ya kujadili na kupitisha humu Bungeni. Miswada hiyo ni ya kuwanufaisha wananchi wa Kenya. Uchanguzi umekaribia. Watu wengine wameamua kutokuja Bungeni kuwashukuru wananchi waliowapigia kura. Wao wameamua kuleta kasheshe humu Bungeni. Namuunga mkono Rais, mia kwa mia. Wembe ni ule ule. Hakuna Rais mwingine ambaye tunatarajia kupitia anga, maji ama nchi kavu. Rais wetu ni Uhuru Muigai Kenyatta."
}