GET /api/v0.1/hansard/entries/756620/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 756620,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/756620/?format=api",
    "text_counter": 144,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Vile vile nashukuru Wakenya wote kwa kuchukua muda wao kuwachagua viongozi mbali mbali ambao wako katika Bunge hili. Nawapongeza Wabunge wenzangu kwa ushindi wao. Pia nashukuru Wakenya kwa sababu walichukuwa fursa yao kumchagua Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto, hata ingawa Korti ilibadilisha hilo. Hiyo sio hoja kwa sababu jambo la maana ni kwamba Kenya imeonekana dunia nzima kuwa nchi inayojali sana usalama na amani. Jambo la maana ni kwamba Kenya imeonekana dunia nzima kama nchi inayojali sana usalama na amani. Kuhusiana na jambo la kubadilisha matokeo ya urais, niliangalia kwa upande mwingine. Niliona kama ni Mungu alikuwa anatumia Uhuru Kenyatta kuonyesha dunia nzima kwamba yeye ni mtu anayeheshimu sheria, na kwamba yeye ni mtu wa amani.Miaka iliyopita, alichukuliwa, pamoja na naibu wake, na kupelekwa katika korti la kimataifa. Akawa Rais Mwafrika wa kwanza kukubali kuenda kwenye korti la kimataifa kujibu mashtaka. Hakusema yeye ni Rais hawezi enda. Alishukisha kiti chake akaachia naibu wake na akapanda ndege akaenda. Mungu akashuka akamfungua minyororo hiyo. Vile vile, Upinzani ulikuwa unangojea kuona Wakenya wakipigana kwa sababu wao walikuwa wanashinda kwa sababu ya karatasi tu, siyo kwa sababu ya kura. Wakaenda kortini na walikuwa wameapa kwamba kama korti ingeamua kwamba Uhuru Kenyatta alishinda vizuri, kungekuwa na vita. Mungu akabadilisha. Akaangalia roho za watu wa Jubilee akaona wao ndio wazuri. Akasema kura irudiwe, na amani ikaendelea kudumu nchini Kenya. Kwa hivyo, tunasema ahsante lakini hatuwezi kupelekwa hapa na pale. Rais amesalimu amri. Amesema turudi kupiga kura tarehe 17 Oktoba, kama ilivyoamuriwa na korti, lakini sisi hatuwezi kukubali hawa jamaa wa Upinzani, wakiongozwa na Raila Odinga, ambaye amekuwa kigeugeu miaka mingi, kutupeleka hapa na pale. Yeye anasema ati sisi hatuwezi kupiga kura tarehe 17 Oktoba. Kwani yeye ni korti kuu? Amesema hawezi kuenda kupigiwa kura. Hiyo ni sawa. Asiende. Hatuna haja naye, lakini juzi alibadilisha kauli yake tena akasema eti kura haitapigwa. Mimi nauliza, ni nani anayepiga kura? Wananchi watapiga kura. Sisi tunataka kusema hivi:Wabunge ambao wako kwa Upinzani na wale ambao wako kwa Serikali, wengi ni wapi? Jubilee imechukua kiasi kikubwa cha viti vya Bunge. Vilevile, tumechukua kiasi kikubwa cha viti vya Seneti. Tumechukua viti vingi katika mabunge ya kaunti, na tunasema tutaendelea. Inafaa wakubali kupiga kura. Wakikataa, sisi tutapiga kura tuendeleze Kenya mbele. Tunataka maendeleo. Kwa hivyo, Raila Odinga ajitayarishe. Tutamshinda na kura nyingi zaidi kwa sababu alikuwa na risasi moja tu. Hata nashangaa Kalonzo Musyoka aliahidiwa kwamba risasi ilibaki moja. Ilitumiwa tarehe nane mwezi wa nane. Sasa nashindwa anangojea risasi gani itumike? Si anangoja ashindwe? Ahsante, Bw. Spika. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}