GET /api/v0.1/hansard/entries/756670/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 756670,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/756670/?format=api",
    "text_counter": 194,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "The Member for Taveta",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Wakenya wengi walipigwa na butwaa tarehe 1 Septemba wakati uamuzi ulipofanywa. Ulikuwa uamuzi wa kuridhisha. Uamuzi wa Mahakama ya Juu haukueleza kwa nini walifanya uamuzi ule. Wakenya wengi wamejiuliza maswali. Nashangaa nikisikia watu wanashangaa kuwa tunashangaa. Ukweli ni kwamba ukifanya uamuzi kama ule kuna umuhimu wa kueleza sababu. Wakenya walitoka kwa wingi tarehe nane mwezi wa nane kwenda kupiga kura ili kuchagua viongozi wao. Sisi ambao tuko hapa tuko kwa njia iliyo halali na tunaambiwa kwamba uchaguzi wa urais ulikuwa hauna uhalali. Vipengele kadhaa katika katiba yetu vimempatia mwananchi nafasi na fursa ya kuchagua viongozi wake. Si sawa kwa uamuzi kama ule kufanywa na tusiambiwe ni kwa nini. Mhe. Spika, vile vile, Wabunge waliochaguliwa katika Bunge hili la 12 wakumbuke kwamba wana jukumu walilopatiwa na wananchi wao ambao walitumia haki yao ya kidemokrasia kuwachagua kuja hapa. Bunge letu la kitaifa lina Wabunge wa pande zote mbili, upande wa walio wengi na upande wa walio wachache. Kawaida kwa sasa hivi walio wachache ni wale ambao wako katika Upinzani. Jamani muangalie msigeuzwe mkawa wanasarakasi ama wanavitimbi kwa sababu upande wa Bunge la Senate, wenzenu wamekwenda wamechagua Spika. Wamerudi leo wamemchagua Naibu wa Spika lakini nyinyi mnaambiwa msifanye masuala yaliyowaleta hapa na haki yenu iliyowaleta hapa na msifanye kazi za wananchi waliowatuma hapa. Wanaowatuma wamewaona nyinyi kama watoto wadogo na hamjui The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}