GET /api/v0.1/hansard/entries/756671/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 756671,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/756671/?format=api",
"text_counter": 195,
"type": "speech",
"speaker_name": "The Member for Taveta",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "mlilokuja kufanya hapa Bungeni. Ninawaomba ndugu zangu mkumbuke umuhimu wa uchaguzi uliotokea na kuwa wananchi waliwapatia nafasi. Mkumbuke kuwa mlipovyokuwa katika kile kinyang’anyiro kulikuwa na wengine pia ambao walikuwa wanastahili kupatiwa nafasi. Wewe ulibahatika kuwa Mbunge wa eneo lako kwa kuweza kuwawakilisha wananchi wako. Nitashangaa sana Wabunge hawa wakienda kwenye vikao vyao kwenye vyama wanashindwa kuwaambia wakubwa wao ukweli uliopo ya kwamba mmetumwa hapa na wananchi waliowachagua. Nawaomba ndugu zangu mkumbuke kuwa Rais Uhuru Kenyatta yuko kwenye kiti kihakika na ndio maanake Wabunge wa Senate wamekwenda kufanya vile wanavyotakikana kufanya. Nyinyi hapa ambao mko wengi kushinda wale mnashindwa nguvu na wachache. Wanawachezea kizungumkuti na mnakubali kuchezewa."
}