GET /api/v0.1/hansard/entries/756672/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 756672,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/756672/?format=api",
"text_counter": 196,
"type": "speech",
"speaker_name": "The Member for Taveta",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Mhe. Spika, ulimwengu una mambo mengi. Unaambiwa unavyozidi kukua ndivyo unavyoona mengi. Kuishi kwingi ndio kuona mengi. Nimechaguliwa sasa kwa mara ya nne na ninajua ya kwamba Mhe. Uhuru Kenyatta mpaka tarehe 17 mwezi wa 10 yuko kwenye kiti kwa njia ya halali na baada ya tarehe 17 tutakuwa tumepatiwa nafasi nyingine ya kuwa na rais ambaye atakalia kile kiti. Nina imani kuwa rais huyo sio mwingine bali ni Uhuru Kenyatta. Naunga mkono masuala yote ambayo rais aliyazungumzia haswa suala la amani, suala la uchaguzi na kuwapongeza kina mama na, nikimalizia, kumpongeza dadangu, Mhe. Teyiaa, kwa kupatiwa nafasi ya kuwa Mbunge katika kaunti ya Kajiado. Mungu awabariki. Tufanye kazi iliyotuleta hapa. Asante sana, Mhe. Spika."
}