GET /api/v0.1/hansard/entries/756890/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 756890,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/756890/?format=api",
    "text_counter": 90,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario Golich Juma",
    "speaker_title": "The Senator for Tana River County",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": " Asante, Bw. Spika. Nachukua nafasi hii kuwashukuru watu wa Tana River County kwa kunichagua kama Seneta wao. Pia ningependa kuwapongeza Maseneta wenzangu waliochaguliwa na walioteuliwa. Ninakupongeza wewe na naibu wako kwa kuchaguliwa kuongoza Seneti hii. Mwisho, ninaipongeza Kamati tekelezi ya Bunge hili kubwa iliochaguliwa. Bw. Spika, nikichangia Hotuba ya Rais wa Kenya ningependa kuunga mkono na kumpongeza juu ya kielelezo chake cha amani, umoja na uwiano. Si vizuri kwetu kama viongozi kugawagawanya Wakenya katika misingi ya kikabila, dini au vyama. Wakati huu ambao tunaelekea uchaguzi wa pili wa Rais inapasa watu wetu wote wahubiri amani ili nchi yetu iendelee. Nchi ya Kenya ni kubwa kuliko mtu mmoja. Kwa sababu hiyo sisi sote tusimame pamoja tuweze kuhimiza watu wetu waishi kwa amani ili nchi yetu ipige hatua za kimaendeleo na tufanye yaliyo mbele yetu kwa amani. Nawasihi wenzangu tuendelee kuhubiri injili ya amani vile Rais alivyoangazia katika hotuba yake. Mwito wangu kwa Wakenya ni tupendane, tushirikiane na tukumbatiane ili tuweze kuelekea mbele kama vile Mhe. Rais alivyosema katika hotuba yake. Kupingana kwetu kusiwagawanye watu wetu na kuweka uhasama kati yao. Hii itatuzuia tusifikie malengo ambayo tunayakusudia. Bw. Spika, ulimi ni kitu nyepesi ambacho kinaweza kuwaweka watu vibaya. Wale wanaotumia ulimi wao vibaya utawaweka katika hali ya aibu. Sisi ni Waafrika; tuna mila, desturi na mwelekeo. Waafrika hawapaswi kuwatukana wazee au viongozi vile alivyotamka Mheshimiwa Babu Owino. Aliwatusi viongozi hasa aliyekuwa mama wa taifa. Tungependa aombe msamaha kwa sababu hiyo inaonyesha nchi yetu kwamba viongozi waliochaguliwa wana maneno ambayo yanaweza kutufanya tuyumbeyumbe. Bw. Spika, hotuba ya Rais ilikuwa ya busara na nia njema kwa Wakenya wote. Wale walio kwa mrengo ule mwingine wanaojitafutia Rais wao wanaweza kufanya hivyo kwa sababu hii ni nchi ya demokrasia ambayo tunafurahia kwa wakati huu. Haifai kutumiwa vibaya kama vile tulivyoshuhudia leo; watu wako barabarani wakiandamana. Vijana wanatumiwa vibaya. Rais wa Kenya amekubali turudie uchaguzi. Uchugazi huo unafaa uwe wa amani lakini vile inavyobainika, wanatuonyesha ya kwamba wanaweza kupiga kelele barabarani, waabiri magari na hiyo haituonyeshi picha nzuri. Bw. Spika, kwa hakika naunga mkono hotuba ya Rais ambayo ni ya busara na nia njema."
}