GET /api/v0.1/hansard/entries/757496/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 757496,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/757496/?format=api",
    "text_counter": 50,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Ali Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Nataka kumpongeza Kiongozi wa Walio Wengi kwa sababu tangu uchaguzi uharamishwe tarehe moja ya mwezi wa tisa, kuna kila aina za habari hapa Kenya. Wengine wametishia eti nchi ya Kenya itavurugika karibuni. Kifungu 140 cha Katiba ya Kenya kinasema iwapo uchaguzi wa Rais utaharamishwa, basi kwa muda wa siku 60, uchaguzi mwingine ufanywe. Sasa babu ameanza yake. Akiamka leo, hataki Safran Morpho; kesho hamtaki Chebukati na kesho kutwa hamtaki Chiloba. Ajue kwamba siku ni 60. Wapende uwapendao na uchukie wale unaochukia lakini sheria imeamrisha, katika Kifungu 140 cha Katiba kwamba, marudio ya uchaguzi wa Rais ufanywe kwa muda wa siku 60. Sasa babu, kama hutaki Chiloba, ni lini tutatangaza hiyo nafasi yake, tupate majibu na tuajiri ili Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) iweze kufanya uchaguzi? Mbona leo unajitia chongo babu? Sheria ni sheria na iko wazi. Akipenda Ali Wario, ama akiichukia babu, sheria iko wazi. Kifungu 142 cha Katiba ya Kenya kinasema kuwa Rais akichagulia, anaanza kazi anapoapishwa na atatoka kwenye hiyo ofisi siku ile rais mwingine ataapishwa. Kwa hivyo kuna kuaapishwa kuwili kwa mjibu wa hicho Kifungu."
}