GET /api/v0.1/hansard/entries/757497/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 757497,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/757497/?format=api",
    "text_counter": 51,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Ali Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Kunao wale wanaoota kule nje na kusema kwamba watafanya maandamano, walete vurugu na kutumia mbinu zozote ili siku 60 zipite. Nia yao ni kuona Serikali ikigawanywa kuwa serikali ya nusu mkate. Ng’o! Kwa bahati mbaya kwao, Kifungu 142 cha Katiba kimeleta suluhu kwa hayo matatizo. Nimesoma Kifungu cha 168 cha Katiba ya Kenya ambacho kinaongea kuhusu wakati kuna malalamiko juu ya Jaji wa Mahakama Kuu. Sheria iko wazi kuhusu hili jambo. Hiki Kifungu kinatambua uhuru wa mahakama. Kimeweka kiwango fulani cha vurugu ndiposa mtu aweze kupeleka malalamishi. Lengo langu halihusiani na hayo. Yaliyotokea tuko na dukuduku nayo na tumekubali hukumu ya mahakama. Basi suluhisho ya hii dukuduku ni nini? Kifungu cha 88(4) kinaielekeza IEBC kwamba kwa siku 60, irudie uchaguzi na wausimamie wao. Siku hizi babu anaamka asubuhi na kusema hataki watu na kampuni fulani, anawataka wengine wafutwe na kampuni fulani ziteuliwe. Sheria iko wazi. Siku ni 60 na wanaosimamia huo uchaguzi ni IEBC wala sio NASA ama babu. Wengi wanataka kuichangia Hoja hii.Naiunga mkono na kumpongeza Kiongozi wa Walio Wengi kwa kuileta. Huko nje kuna vitisho vya kila aina. Ili tuondowe hivyo vitisho, IEBC ilete kura tarehe 26 ili tufunge hii hesabu na twende nyumbani. Maneno ya babu yametuchokesha kichwa. Ahsante, Mhe. Spika. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}