GET /api/v0.1/hansard/entries/757528/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 757528,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/757528/?format=api",
    "text_counter": 82,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Limo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1915,
        "legal_name": "Joseph Kirui Limo",
        "slug": "joseph-kirui-limo"
    },
    "content": "Ahsante sana Mhe. Spika. Ningependa kumshukuru Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni kwa kuleta hii Hoja ambayo ina maana sana. Kuhusu maneno ambayo yanaendelea nchini, haitakikani sisi Wabunge kujifanya hatujui ni nani analeta shida. Hii shida inajitokeza kwa sababu moja tu: mtu fulani hajashinda uchaguzi. Huyo mtu ni huyu jamaa ambaye alikuwa anaitwa Agwambo halafu akabadilisha sasa anaitwa Baba. Sijui ni baba bandia ama nini. Juzi amejibadilisha tena. Sasa anajiita Joshua. Sijui ni Joshua bandia pia ama nini. Baadaye tena amebadilika akawa ni kompyuta. Eti sijui yeye ni kifaranga. Nchi yetu haiwezi kuendeshwa kwa namna hiyo. Lazima wananchi wa Kenya wajue kwamba nchi ni yetu sisi sote. Nchi siyo ya mtu mmoja. Mhe. Spika, kwa hivyo, kuitisha eti kompyuta ifunguliwe iangaliwe ndani, sisi Wabunge tusijifanye tunataka kubadilisha sheria nusu nusu. Tubadilishe sheria inayohusu uchaguzi wa Kenya. Tusijifanye eti kwamba tunapitisha sheria ya uchaguzi kuufanya uwe digital na hali sivyo. Maanake ukienda kupiga kura, kwanza unaguza mitambo ya kompyuta ili utambuliwe kama mpiga kura. Halafu unachukua karatasi ya kupigia kura kuandika kwa mkono wako na unaweka kura kwenye sanduku ukitumia mkono vile vile. Baada ya kupiga kura, unaambiwa eti kura yako inawekwa kwenye kompyuta ndiyo ipite hewani mpaka Bomas of Kenya. Tunataka tujaze hiyo fomu inaitwa 34B na tuilete moja kwa moja mpaka Bomas of Kenya, kisha tuhesabu kama tulivyokuwa tukifanya zamani. Tuache maneno ya kusema kompyuta. Hatujaenda kompyuta, Mhe. Spika. Tunataka tubadilishe sheria katika hili Bunge. Tusiibadilishe nusu. Tuibadilishe ili tuwe na uchaguzi wa maandishi hatimaye tulete kura mpaka Bomas of Kenya na tuzihesabu. Mambo ya kompyuta ipotee!"
}